Na Ummy Muya
NAIBU Waziri wa Kazi Ajira na Maendeleo ya Vijana Dkt Milton Mahanga amesema kuwa mkoa wa Dar es Salaam ni wa pili kwa maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi ikitanguliwa na mkoa wa Iringa.
Mahanga alisema hayo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa katika hala fupi ya maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani. Maadhimisho hayo, kitaifa yalifanyika mkoani Kigomana
Hata hivyo, alisema kuwa takwimu za kitaifa zinaonyesha kuwa maambukizi ya ukimwi yamepungua kutoka asilimia 7 hadi kufikia 5.8.
“Elimu ya ukimwi kwa vijana inasaidia kujiamini, kujikinga na kujiepusha na maambukizi ya ugonjwa hup ambao mpaka sasa chanjo na tiba bado ni kitendawili”alisema Mahanga.
Alisema kutokana na tatizo hilo bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania mwanzoni mwa mwaka huu lilipitisha sheria ya ukimwi ambayo lengo lake kubwa ni kuwadhibiti wagonjwa wa ukimwi wanaoeneza ugonjwa huo kwa makusudi.
Katika hatua nyingine, Watanzania wameshauriwa kutobweteka na takwimu zinazoonyesha kuwa ugonjwa wa Ukimwi umepungua na badala yake waongeze kasi ya kupambana nao, anaripoti Boniface Meena.
Ushauri huo ulitolewa jana na Mkurugenzi wa Shirika la kupambana na Ukimwi (TAYOA), Peter Masika, wa kati akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni ya siku 30 za Kituo cha Youthbalozi kupambana na Ukimwi.
"Tusisubiri mpaka hali ikawa mbaya sana lazima tuwe na mikakati ya kuutokomeza Ukimwi, hizi takwimu zisitufanye tupumzike mapambano bado yanaendelea," alisema Masika
Wakati huo huo, Mtaalamu wa Maabara wa kitengo cha damu salama Kanda ya Mashariki Ndeonisia Towo, amewataka Watanzania kujitokeza kupima afya zao ili kujua maambukizi ya Ukimwi na kushiriki katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo, Geofrey Nyang'oro.
Towo alitoa wito huo alipokuwa akizungumza na jijini Dar es Salaam juzi ambapo pia alitaja chanzo cha watu kuhofu kupima afya zao kuwa ni kutokuwa waaminifu katika ngono.
"Watu wengi wanashindwa kujitokeza kupima afya zao kutokana na kutokuwa na uhakika na mienendo yao na hali hii ni hatari kwa kuwa inawafanya wakate tamaa na waendelee na vitendo vinavyochangia maambukizi ya VVU," alisema.
Aliwataka watu kuachana na mawazo kama hayo na badala yake kujitokeza kupima ili kujua hali ya afya zao kwani kufanya hivyo kutawafanya waishi kwa uhuru na kwa uhakika kuliko wakiishi kama hivi walivyo.
Naye Festo Polea anaripoti kuwa wastani wa watoto 2.3 milioni waliopo chini ya miaka 15, wanaumwa ugonjwa wa ukimwi, huku watoto 15.2 milioni wamepoteza mzazi mmoja ama wote.
Takwimu hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Programu wa Shirika lisilo la kiserikali la Plan Tanzania, Nene Sow Thiam, wakati wafanyakazi wa shirika hilo walipokuwa wakitoa msaada mbalimbali kwa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Watoto Yatima cha Taifa, Kurasini.
Alisema takwimu zilizofanywa na shirika hilo zinaonyesha kuwa asilimia 50 ya watoto walioambukizwa Ukimwi, wapo katika hatari ya kufa mapema endapo hawatapata dawa na huduma zinazostahili.
-
No comments:
Post a Comment