Friday 18 September 2009

SALAM ZA SIKUKUU YA IDD EL-FITRI TOKA KWA MHESHIMIWA BALOZI MWANAIDI SINARE MAAJAR


Ndugu Watanzania wenzangu,


Ninayo furaha kubwa kuwatumia Mkono wa Idd El-fitri, mwaka huu wa 2009.  Kwa niaba ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kwa niaba ya wafanyakazi wenzangu katika Ubalozi wa Tanzania London, na kwa niaba yangu binafsi, napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza kwa kumaliza salama mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Nawatakieni nyote kila la kheri wakati huu wa sikukuuu.


Idd Mubarak

No comments: